Uganda
Huwezi kusikiliza tena

Washtakiwa saba wapatwa na hatia Uganda

Jaji nchini Uganda amewakuta na hatia ya ugaidi, mauaji na jaribio la mauaji watuhumiwa saba wa mashambulizi mawili ya mabomu wakati wa michuano ya kombe la Dunia ya mpira wa miguu mjini Kampala mwaka 2010. Zaidi ya watu sabini waliuawa.

Watuhumiwa wengine sita wamefutiwa mashtaka hayo. Akiegemea kwenye ushahidi uliokwishatolewa, Jaji Alfonse Owiny-Dollo amemkuta Isa Ahmed Luyima kuwa ndiye kinara kwa niaba ya kundi la al Shabab. Washtakiwa hao - Wakenya sita, Waganda watano na Watanzania wawili walisema waliteswa ili kukiri makosa, madai ambayo mahakama ya Uganda imeyakanusha.

Siraj Kalyango ana maelezo zaidi.