hamasa kuhusu umuhimu wa hedhi Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Hamasa kuhusu umuhimu wa hedhi yafanywa TZ

Siku za hedhi huhitaji mazingira ya faragha kubwa na usafi, nchini Tanzania imeelezwa kuwa wasichana hupoteza mpaka siku 5 kwa kutokwenda shule kutokana ukosefu wa vyoo na maji safi hali inayochangia wanafunzi hao kukosa uhuru na kuamua kubakia nyumbani .Katika maadhimisho ya mwaka huu Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali wa Serikali na Asasi za kiraia kwa lengo la kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa Hedhi Salama. Mwandishi wetu Liz Masinga alihudhuria shamra shamra hizo na kukutana na mabinti wakaeleza namna walivyojifunza..