Huwezi kusikiliza tena

Video: Kijana aliyepotea Japan apatikana

Mvulana mwenye umri wa miaka saba,Yamato Tanooka aliyepotea nchini Japan Jumamosi iliyopita sasa amepatikana akiwa hai.

Maafisa wa utawala katika kisiwa cha Hokkaido wanasema alipatikana na mwanajeshi mmoja katika kituo cha kufanyia mazoezi nje ya mji wa Shikabe mnamo Ijumaa.

Kijana huyo huyo ambaye aliachwa na babake mwituni kama adhabu alitembea kwa zaidi ya kilomita 4 hadi ukingo wa msitu huo alikotulia.