Muhammud Ali
Huwezi kusikiliza tena

Bondia aliyepigana na Muhammud Ali Kenya

Aliyekuwa bondia wa kimataifa nchini Kenya Muhammad Abdallah Kent anasema kuwa ameshangazwa na kifo cha Muhammud Ali na hakuweza kujizuia machozi yake wakati dadake alipompingia simu na kumueleza kuhusu kifo chake.Kent aliiwakilisha Kenya kutoka mwaka 1973 hadi 1986,mara ya kwanza akiwa katika uzani wa kati na baadaye katika uzani mzito.Alipigana na Ali katika pigano la raundi nne mwaka 1980 mjini Nairobi wakati Ali alipozuru Afrika kuyashawishi baadhi ya mataifa kujiondoa katika michezo ya Olimpiki ya Moscow baada ya Sovieti kuvamia Afghanistan.John Nene ameandaa taarifa ifuatayo