Pogba kufanyiwa vipimo vya afya Manchester United

Paul Pogba Haki miliki ya picha PA
Image caption Pogba alichezea United mwisho dhidi ya Wolves Machi 2012

Klabu ya Juventus ya Italia imemruhusu mshambulizi wake Paul Pogba kufanyiwa vipimo vya afya Old Trafford katika moja ya ishara kuwa huenda Manchester United imeafikiana na wakala wake kumnunua mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa likizoni Marekani baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2016.

Pogba, 23, amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford kwa bei ya kuvunja rekodi ya dunia ya ununuzi wa wachezaji ya pauni milioni moja.

Pogba alichezea United mwisho dhidi ya Wolves Machi 2012

Akiwa Old Trafford Pogba alichezeshwa katika mechi 3 pekee.

Meneja wa United Jose Mourinho alikuwa amedokeza kwamba klabu hiyo ilikuwa imekaribia sana kumpata Pogba.

"Kwa sasa, Pogba ni mchezaji wa Juventus," amesema Allegri.

United wataanza msimu kwa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester City Jumapili.

Juventus wataanza msimu wao Serie A wiki moja baadaye tarehe 20 Agosti.