Nigeria yafuzu kwa robo fainali Rio

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Super Eagles ya Nigeria imefuzu kwa robo fainali ya olimpiki Rio

Wawakilishi wa Afrika katika kandanda ya Olimpiki ,Super Eagles ya Nigeria wamefuzu kwa robo fainali ya olimpiki mjini Rio baada ya kushinda mechi yao ya pili dhidi ya Sweden.

Sadiq Umar ndiye aliyefunga bao la pekee na la ushindi kwa mabingwa hao wa 1996.

Katika mechi ya kwanza Super Eagles waliwabana Japan 5-4 katika mechi iliyochezwa saa chache tu baada ya kutua Brazil kufutia hitilafu ya usafiri kutoka marekani hadi Brazil.

Nigeria sasa wanajiandaa kwa mechi ijayo dhidi ya Colombia siku ya Jumanne.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii