Ryan Lochte apoteza mikataba minne ya udhamini

Kampuni ya uogeleaji ya Speedo ilikuwa ya kwanza kusitisha mkataba wake
Image caption Kampuni ya uogeleaji ya Speedo ilikuwa ya kwanza kusitisha mkataba wake

Muogeleaji wa Marekani Ryan Lochte amepoteza mikataba yake yote minne ya udhamini baada ya wenzake watatu kudanganya kuwa waliibiwa na wezi waliokuwa na silaha katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika mjini Rio.

Kampuni ya uogeleaji ya Speedo ilikuwa ya kwanza kusitisha mkataba wake ikifuatiwa na Luxury retailer, Ralph Lauren, The Skin Care company,na Kampuni ya matress na Airweave.

Lochte bado anakabiliwa na mashitaka ya kujibu kwa mamlaka ya michezo nchini Brazil ikiwa ni uhalifu pamoja na utovu wa nidhamu.

Image caption Lochte bado anakabiliwa na mashitaka ya kujibu kwa mamlaka ya michezo nchini Brazil

Mwandishi wa BBC amesema kuwa muogeleaji huyo anaweza kutokushiriki kabisa mashindano mengine ya kuogelea.