Urusi yajibu baada ya kufungiwa kushiriki michezo ya walemavu

Waziri mkuu wa Urusi,Dmitry Medvedev, amesema kwamba uamuzi huo ni wa kijinga
Image caption Waziri mkuu wa Urusi,Dmitry Medvedev, amesema kwamba uamuzi huo ni wa kijinga

Urusi Imejibu kwa kauli nzito maamuzi ya mahakama moja ya kupiga marufuku ushiriki wa wanamichezo walemavu kutoka nchini Urusi , sababu kubwa ikitajwa kuwa ni utumizi wa dawa za kusisimua misuli na masharti waliyoyaweka na wadhamini.

Waziri mkuu wa Urusi,Dmitry Medvedev, amesema kwamba uamuzi huo ni wa kijinga na kwamba ni pigo kwa watu wote wenye ulemavu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanamichezo walemavu kutoka Urusi nao wametoa kauli nzito kufuatia madai hayo

Hata hivyo ametupilia mbali uchunguzi wa hoja ya dawa za kulevya kwa Urusi na kudai kwamba ni sawa na usaha,na ndani yake kuna msukumo wa kisiasa na mchanyato wa machukizo kwa wakati mmoja.

Mahakama ya Usuluhishi katika masuala ya michezo imezingatia marufuku hiyo kwa sababu na kusema kwamba Urusi haijawasilisha ushahidi wowote kupinga madai hayo.

Wanamichezo walemavu kutoka Urusi nao wametoa kauli nzito kufuatia madai hayo na mmoja wao kuuelezea uamuzi huo kama wa kufedhehesha.