Mkuu wa FIFA wa zamani Sepp Blatter mahakamani tena

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bw Blatter anahudhuria mahakamani kusikiliza kesi hiyo inayoendeshwa na mahakama ya usuluhishi wa mizozo katika michezo nchini Uswizi.

Rais wa zamani wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA Sepp Blatter, anawasilisha rufaa yake ya mwisho mahakamahi hii leo dhidi ya marufuku aliyowekewa ya michezo na michezo kwa kukiuka madili.

Bw Blatter anahudhuria mahakamani kusikiliza kesi hiyo inayoendeshwa na mahakama ya usuluhishi wa mizozo michezoni nchini Uswizi.

Akizungumza na maripota mjini Lausanne, amejielezea kama mtu mwenye matumaini.

Bw Blatter aliwekewa marufuku hiyo mwezi Disemba mwaka jana kwasababu aliidhinisha malipo ya zaidi ya dola milioni mbili kwa mkuu wa zamani wa soka barani Ulaya , Michel Platini, miaka mitano iliyopita.

Mwezi Mei, Bw Platini alishindwa kushawishi kuondolewa kwa marufuku dhidi yake, ingawa ilipunguzwa kutoka miaka sita hadi miaka minne.