Serena Williams ashindwa US Open na kupitwa na Mjerumani

Serena Williams Haki miliki ya picha Reuters

Mchezaji tenisi mashuhuri Serena Williams ameondolewa kutoka kwenye mashindano ya wazi ya US Open jijini New York baada ya kushindwa hatua ya nusufainali.

Ameshindwa na mchezaji wa Jamhuri ya Czech Karolina Pliskova 6-2 7-6 (7-5).

Mchezaji huyo aliyeorodheshwa nambari moja duniani alikuwa anatumai kuweka rekodi kwa kushinda tuzo ya grand slam mara ya 23.

Lakini kwa sasa atasalia kushikilia rekodi na mchezaji wa zamani Steffi Graf katika mataji 22.

Matokeo hayo yana maana kwamba Serena Williams, 34, sasa atapitwa kwenye orodha ya wachezaji bora na Mjerumani Angelique Kerber.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kerber amefika fainali mara ya tatu 2016

Mjerumani huyo alimshinda raia wa Denmark Carolina Wozniacki 6-4 6-3.

Pliskova atakutana na Kerber kwenye fainali.