Wenger: Laurent Koscielny ni beki stadi

Wenger Haki miliki ya picha Getty Images

Meneja wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger amesema beki wa kati wa klabu hiyo Laurent Koscielny ni miongoni mwa wakabaji bora zaidi duniani.

"Hakuna mchezaji ambaye huwezi kupata mbadala, lakini yeye amefikia hadhi tofauti kwetu. Ana uzoefu na anajiamini sana," amesema Wenger.

Meneja huyo pia amefichua kwamba Koscielny yuko sawa kucheza dhidi ya miamba wa Ufaransa Paris St-Germain mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baadaye Jumanne jioni.

"Amejijengea jina katika soka ya Uingereza. Nafikiri yeye ni miongoni mwa wale bora zaidi duniani. Natumai atadhihirisha hilo dhidi ya PSG."

Koscielny, 31, ambaye ni nahodha msaidizi Arsenal pia huchezea timu ya taifa ya Ufaransa.