Man United yashindwa kwa mara ya tatu mfululizo

Watford waicharaza Man United 3-1
Image caption Watford waicharaza Man United 3-1

Klabu ya Manchester United imeshindwa kwa mara ya tatu mfululizo katika kipindi cha juma moja baada ya mabao ya mda wa lala salama kutoka kwa mshambuliaji Juan Zuniga,Troy Deeney kuipatia ushindi Watford .

Watford iliongoza baada ya Etienne capoue kufunga kutoka kwa krosi iliopigwa na Daryl Janmaat kabla ya Marcus Rashford kusawazisha.

Lakini mchezaji wa ziada Zuniga alifunga ikiwa imesalia dakika saba mchezo kukamilika.

Deeney baadaye alifunga penalti katika mda wa ziada baada ya Marouane Fellaini kuangushwa katika ebeo hatari.

Hii ni mara ya tatu mfulilozi kwa Manchester United kupoteza,ikishindwa 2-1 na Manchester City,baadaye ikapoteza 1-0 dhidi ya klabu ya feyenoord ya Uholanzi katikati ya wiki katika kombe la bara Ulaya.