Tanzania mabingwa wa Cecafa 2016 upande wa wanawake

Tanzania
Image caption Tanzania walifika fainali baada ya kuwalaza wenyeji Uganda nusu fainali

Kilimanjaro Queens wa Tanzania ndio mabingwa wa Cecafa upande wa kina dada 2016 baada ya kulaza Harambee Starlets wa Kenya 2-1 mjini Jinja, Uganda.

Magoli ya Tanzania yamefungwa na Mwahamisi Omar dk 28, 45, Kenya limefungwa na Christina Nafula.

Tanzania walifika fainali baada ya kuwalaza wenyeji Uganda 4-1 mechi ya nusu fainali.

Kenya walifika fainali kwa kuwalaza Ethiopia 3-2.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Kilimanjaro Queens wa Tanzania wakisherehekea ushindi Cecafa
Image caption Mashabiki wa Kenya