Perez afungia Arsenal mabao ushindi dhidi ya Nottingham Forest

Lucas Perez Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ilikuwa mara ya pili kwa Lucas Perez kuanza mechi Arsenal tangu ajiunge nao kutoka Deportivo La Coruna mwezi Agosti

Lucas Perez alifungia klabu ya Arsenal mabao yake ya kwanza na kuwasaidia Gunnerskupata ushindi mkubwa dhidi ya Nottingham Forest na kufika raundi ya nne Kombe la Ligi Uingereza (EFL).

Granit Xhaka aliwaweka Arsenal kifua mbele kwa kombora la hatua 30 kutoka kwenye goli dakika ya 23.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nicklas Bendtner alishindwa kufunga penalti upande wa Forest kabla ya Lucas kuongeza ushindi wa Arsenal kupitia mkwaju wa penalti baada ya Chuba Akpom kuchezewa visivyo dakika ya 60.

Lucas kisha alimbwaga kipa na kufunga bao lake la pili usiku huo dakika ya 71 kabla ya Alex Oxlade-Chamberlain kukamilisha ushindi wao dakika ya 93.

Ilikuwa mara ya pili kwa Lucas Perez kuanza mechi Arsenal tangu ajiunge nao kutoka Deportivo La Coruna mwezi Agosti

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nicklas Bendtner alijiunga na Nottingham Forest 7 Septemba kutoka Wolfsburg ya Ujerumani

Nicklas Bendtner alijiunga na Nottingham Forest 7 Septemba kutoka Wolfsburg ya Ujerumani.

MECHI NYINGINE ZA JUMANNE 20 SEPTEMBA 2016

  • Bournemouth 2-3 Preston
  • Brighton 1-2 Reading
  • Derby 0-3 Liverpool
  • Everton 0-2 Norwich
  • Leeds 1-0 Blackburn
  • Leicester 2-4 Chelsea
  • Newcastle 2-0 Wolves
  • Nottm Forest 0-4 Arsenal