Utafiti: Farasi wanaweza kuwasiliana na binaadamu

farasi
Image caption Farasi

Farasi wamejumuishwa miongoni mwa wanyama ambao wanaweza kuwasiliana kwa ishara.

Wanasayansi waliwafunza farasi kwa kuwapatia karoti kama motisha kugusa ubao na pua ili kubaini iwapo wangependa kuvaa blanketi

Ombi la farasi hao lilikwenda kulingana na hali ya hewa,ikimaanisha kwamba halikuwa chaguo la kawaida.

Wanyama wachache wakiwemo sokwe na pomboo huwa kama wanadamu wakati wanapoonyesha kitu kwa ishara.

Daktari Cecilie Mejdel wa taasisi ya wanyama nchini Norway ,ambaye aliongoza utafiti huo ,alisema kuwa walitaka kutafuta njia ya kuwauliza farasi iwapo walipendelea kuvaa blanketi au la.

"farasi hutambulika kuwa mnyama asiyetumia akili sana,lakini utafiti huu unaonyesha kuwa kwa kutumia njia zilizo sawa wanaweza kuwasiliana na kuonyesha hisia zao na pia wanaweza kuchagua kitu kilicho na busara kwa wanadamu.