Gareth ajipongeza kuiongoza England

Gareth Southgate Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Southgate

Kaimu meneja wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate amesema 'ilikuwa hatua muhimu' kuchukua nafasi ya meneja wa zamani Sam Allardyce.

Southgate, ambaye wakati wa uchezaji wake alikuwa beki, awali amekuwa akinoa timu ya vijana chipukizi wenye chini ya umri wa miaka 21 na ataongoza klabu hiyo ya taifa ya Uingereza kwa michuano minne ijayo.

Allardyce aling'atuka siku ya Jumanne baada ya uchunguzi wa gazeti la Daily Telegraph kudai kuwa Allardyce, alitumia cheo chake kushiriki mpango wa pauni 400,000 na kutoa ushauri kuhusu vile watu wangeweza ''kukwepa'' sheria za uhamiaji wakati wa kuhama kwa wachezaji.

Southgate, 46, amesema mwezi Juni hakuwa na matamanio yoyote ya kumrithi Roy Hodgson kama meneja wa timu hiyo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Arsenal Arsene Wenger

Hata hivyo meneja wa Arsenal Arsene Wenger na Eddie Hodgson wa Bournemouth ambao wamehusishwa na matamanio ya kazi hiyo wameelezea jitihada zao kwa klabu zao.

Meneja wa Uingereza amesema nafasi hiyo ni kama 'wadhifa mkubwa', huku wenger amesema 'anaangazia' klabu ya Arsenal kwa asilimia 100

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii