''Busu'' lamuepusha kupigwa marufuku michezo ya Olimpiki

Shawn Barber Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shawn Barber

Bingwa wa dunia katika mchezo wa kuruka kwa kutumia ufito {Pole Vaulter} Shawn Barber alikuwa na haki ya kushiriki katika michezo ya Olimpiki licha ya kugunduliwa kwamba alitumia dawa ya Cocaine aliyokula wakati alipokuwa akishiriki ngono.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 22 aliepuka marufuku ya miaka miwili akidai kwamba alipata dawa hiyo kupitia busu.

Jopo huru liliamua kwamba Barber ambaye alimaliza wa 10 mjini Rio hakufanya makosa yoyote.Shirika la riadha nchini Canada lilitaja hatua hiyo kuwa ya ''haki na busara''.

Barber alichapisha tangazo katika mtandao wa kijamii akitafuta mwanamke ambaye alikuwa hatumii dawa za kulevya na asiye na ugonjwa wowote usiku wa kuamkia majaribio ya wanariadha wa Canada.

Aliibuka mshindi na kuweka rekodi mpya ya kitaifa lakini atalazimika kuzipoteza.

Barber anadai kwamba alitaka kushiriki ngono ili kuondoa msongo wa mawazo.

Mwanamke aliyekuwa naye anasema kuwa alikula Cocaine na wakati walipokutana alimpinga busu mara kadhaa bila ya kumweleza kwamba alikuwa ametumia dawa ya kulevya.