Nicola Adams anatafakari kushiriki masumbwi kitaaluma

Nicola Adams mshindi mara mbili wa masumbwi katika Olimpiki kutoka Uingereza Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nicola Adams mshindi mara mbili wa masumbwi katika Olimpiki kutoka Uingereza

Mshindi mara mbili wa Olimpiki Nicola Adams anasema amefanya mazungmo kuhusu kupigana masumbwi kama taaluma.

Adams amekuwa mpiganaji masumbwi wa kwanza kushinda medali ya dhahabu aliposhinda katika mashindano ya London 2012.

Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 33 kutoka Yorkshire alishinda uzani wa flyweight katka mashindano ya Rio mwaka huu, akiwa mwanamasumbwi wa kwanza wa Uingereza kutetea taji lake la olimpiki katika muda wa miaka 92.

Alipoulizwa kuhusu maisha yake ya mebeleni, ameiambia BBC: "iwapo nitaishia kupigana ki taaluma, nitaweka tofuati kubwa."

Adams ameongeza : " nimefanya mazungumzo kiasi na mapromota kadhaa na bado nahitaji kufikiria kuhusu ninachotaka kufanya kwa kweli.

"kuna mashindano ya Olimpiki ya Tokyo ambayo pia ningependa kushiriki, lakini kugeuka kuwa mwanamasumbwi kitaaluma ni changamoto kubwa. Nani anayejua huedna tuakwana bingwampya wa dunia."

Adams aliangazia kipindi cha ufanisi cha mshindi wa medali ya shaba katika olimpiki kwenye mchezo wa Judo, Ronda Rousey aliyeingilia mchezo wa Martial Arts, na akashinda taji la UFC duniani uzito wa bantam.

Adams aliulizwa kuhusu bingwa wa masumbwi duniani uzani mzito Tyson Fury kutoka Uingereza, ambaye huenda akapoteza kibali chake cha kushirika masumbwi baada ya kufichua kuwa alitumia bangi katika kujaribu kukabiliana na msongo wa kimawazo.

Fury, mwenye umri wa miaka 28, alidai pia alistaafu Octoba 3, na kuishia kupinga kauli hiyo saa tatu baadaye.

"kwa timu ya Uingereza tuna kila kitu; madakatari, wataalamu wa lishe bora, wanasaikolojia - na hatuna haja ya kuwana wasiwasi kuhusu chochote," Adams amesema.

"labda kuna haja ya kuwana hayo katika taaluma ya mchezo huo, mtu ambaye wanamsumbwi wanaweza kuzungumza naye."