San Marino washerehekea licha ya kushindwa 4-1

San Marino Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption San Marino walicheza mechi ya kwanza ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 1992

Timu ya San Marino ilisherehekea kufunga bao la kwanza la ugenini katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia katika kipindi cha miaka 15, licha ya kulazwa 4-1 na Norway.

Bao la kusawazisha la Mattia Stefanelli dakika ya 54 liliwajaza furaha raia wa nchi hiyo walishangilia sana.

Kwenye ukurasa rasmi wa Twitter wa mashabiki wa timu hiyo, jina bao liliandikwa kwa kuvuta 'A' sana .

Norway hata hivyo walifunga mabao mengine matatu katika kipindi cha dakika saba na kuondoka na ushindi mkubwa.

Lakini furaha ya San Marino haikukomea hapo, huku kwenye ukurasa uo huo wa Twitter timu hiyo ikisema huenda wakasubiri miaka mingine 15 kupata bao jingine la ugenini.

San Marino wameorodheshwa namabri 201 na Fifa.