Wataka uvuvi kushirikishwa katika Olimpiki

Wataka mchezo wa uvuvi kushirikishwa katika Olimpiki Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wataka mchezo wa uvuvi kushirikishwa katika Olimpiki

Shirika la kimataifa kuhusu uvuvi limewasilisha ombi la kushirikisha uvuvi katika michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

Shirikisho la kimataifa la mchezo wa uvuvi limesema kuwa kukubali uvuvi katika michezo ya Olimpiki kutaongeza idadi ya michezo katika Olimpiki kwa sababu mchezo huo ni maarufu sana.

Samaki wanaoshikwa watarudishwa katika maji bila kupata madhara yoyote.

Lakini wakosoaji wanasema kuwa uvuvi unashirikisha bahati kubwa na unachosha kutazama.

Wanapinga maoni ya rais wa mchezo huo Ferenc Szalay kwamba mchezo huo unaafikia maadili ya michezo ya Olimpiki.

Kuteleza kwa kutumia ubao,kuteleza majini,Kucheza karate pamoja na baseball/softball imekubalika katika michezo ya 2020.

IOC imesema kuwa inatumaini hatua hiyo itawavutia mashabiki kupitia kushirikisha michezo inayowavutia vijana.