Mchezaji wa Nigeria apigwa risasi na kufariki

Mchezaji wa shooting Stars nchini Nigeria Izu Joseph kushoto
Image caption Mchezaji wa shooting Stars nchini Nigeria Izu Joseph kushoto

Mwanasoka mmoja anayesakata dimba katika michuano ya ligi ya Nigeria, amepigwa risasi na kufariki nyumbani kwake katika jimbo la Bayelsa kusini mwa nchi hiyo.

Mwaandishi wa BBC anasema kuwa Izu Joseph, beki wa timu ya Shooting Stars, aliuawa na askari waliokuwa wakikabiliana na wanamgambo katika eneo lenye utajiri wa mafuta.

Miezi ya hivi karibuni kumeshuhudiwa mapigano mapya katika eneo la Delta, huku wapiganaji wakitaka kupewa sehemu ya utajiri wa mafuta.