Guardiola: 'Mustakabali wa Aguero na Kompany upo ManCity'

Pep Guardiola Haki miliki ya picha Rex Features

Mkufunzi wa timu ya Manchester City Pep Guardiola anasema Sergio Aguero na Vincent Kompany wote wana miaka ya ziada katika klabu hiyo ya ligi ya Uingereza.

Wote hawakucheza katika mchuano wa ligi ya ubingwa wa Ulaya dhidi ya Barcelona ambapo Man City ilifungwa.

Kompany hakuwepo hata kwenye benchi, jambo lililozusha tuhuma kwamba huyenda wanasoka hao hawapo katika mipango ya Guardiola.

Lakini kocha huyo wa Uhispania amesema: "Vincent alikuwa hayuko sawa kucheza. Sergio, nilisema baada ya mechi, ilikuwani uamuzi wa kiufundi.

"Iwapo Sergio ataamua kuondoka, utakuwa ni uamuzi wake."

Guardiola amethibitisha Pablo Zabaleta na Bacary Sagna wote watakosa mchuano wa Jumapili wa Premier League dhidi ya Southampton katika uwanja wa Etihad kutokana na majeraha.

Haki miliki ya picha Getty Images

Uamuzi wake kutomchezesha Aguero na Kompany umezusha maswali, kama ilivyo kwa utendaji wa kipa Claudio Bravo, aliyeondolewa Nou Camp, na mbinu yake ya kumiliki mpira, ambayo Guardiola amesema mara kwa mara hatoibadili imezusha shutuma.

"Mustakabali wa Vincent na Sergio upo Manchester City. Atakapokuwa sawa, ni mchezaji mzito wa kiungo cha ulinzi. Nampenda. Katika suala la Aguero, ulikuwani uamuzi wa kifundi. Nilitaka mchezaji mmoja wa ziada wa kiungo cha kati . Najaribu kuudhibiti mpira, kwasababu ukiwa nao, Lionel Messi, Neymar na hata Luis Suarez hawaupati.