Bondia wa Tanzania anayeuza matunda
Huwezi kusikiliza tena

Bondia wa Tanzania anayeuza matunda

Lulu Kayage ni msichana wa Kitanzania wa umri wa miaka 24 ambae ni bondia , Lulu ameamua kuwa mjasiriamali kwa kuuza genge la matunda kutokana na kuwa mchezo wa masumbwi haulipi.

Hata hivyo licha ya mchezo kutokulimpa siku chache zijazo atapanda ulingoni nchini ya Africa ya kusini kuwania ubingwa wa Afrika uzani wa Bantam kwa kupigana na Bondia Leighandre Jegels almarufu Baby jay

Mwandishi wetu Omary Mkambara alimtembelea bondia huyu katika biashara yake na kisha kuambatana mpaka mazoezini na hii ni taarifa yake