David Moyes apigwa marufuku mechi moja na FA

David Moyes Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sunderland wanashika mkia Ligi ya Premia

Meneja wa Sunderland David Moyes amepigwa marufuku mechi moja na chama cha soka cha England kwa kutumia lugha ya matusi dhidi ya mwamuzi wa mechi.

Aidha, amepigwa faini ya £8,000.

Kisa hicho kilitokea baada ya refa kunyima Sunderland mkwaju wa penalti dakika ya 90 mechi ya Jumatano wiki iliyopita ambapo klabu hiyo ilishindwa 1-0 na Southamptn Kombe la FA.

Baada ya mechi hiyo, Moyes alisema: "Tatizo lilitokea aliponiandama hadi pahala nilipokuwa nimesimama. Nilitumia lugha ya matusi na sikufaa kufanya hivyo."

Sunderland watacheza na Bournemouth Ligi ya Premia Jumamosi.

Moyes aliteuliwa meneja wa Sunderland Julai na ameshinda alama mbili pekee kutoka kwa mechi 10 ligini.