Kompany hana jeraha lolote

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vincent Kompany

Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany hana jeraha lolote, licha ya kutolewa kwake katika mechi waliotoka sare ya bao moja kati ya Ubelgiji na Uholanzi.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 30 , amepata majeraha kwa misimu ya hivi karibuni na kujitoa kwa muda kabla mechi ya Jumatano.

''Hana jeraha lolote,''amesema meneja Roberto Martinez. Hatukutaka kuchukua tahadhari yoyote kwake na Kompany alikuwa anajihisi vibaya baada ya mazoezi.

Huku ,mshambuliaji wa Tottenham Vincent Janssen alipata mshtuko katikati ya mchezo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 , amefunga mabao mara nne kwa timu ya spurs tangu uhamisho wake kutoka AZ Alkmaar kwa thamani ya dola milioni 17.

Janssen,alitolewa uwanjani katika awamu ya kwanza ya mchezo baada ya kugongana na mlinda lango wa Ubeligiji Simon Mignolet.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Ujumbe wa Simon Mignolet kwa Janssen

Kompany ilibidi aombe msaidizi wakati wa mapumziko katika mechi yao dhidi ya Manchester united mwezi uliopita kwa sababu ya 'uchovu'.

Meneja Pep Guardiola amesema Kompany bado ana siku katika klabu hiyo lakini anahitaji imani kucheza mara kwa mara'' baada ya kuuguza majereha kwa mfululizo.

Beki huyo wa kati alitajwa miongoni mwa watakaoshiriki mechi ya kirafiki siku ya Jumatano huko Amsterdam,lakini akabadilishwa na Christian Kabasele kutoka Watford.

Kompany kwa hivi sasa hajulikani iwapo atashiriki mechi za kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Estonia siku ya Jumapili.

'Ninataka kila mchezaji kuwa asilimia 100,''amesema Martinez . Nitashtuka iwapo atacheza siku ya Jumapili , lakini ni mapema sana kusema hilo.

Tutahitaji kuangazia hali ilivyo , haswa na klabu yake. Iwapo hayuko tayari nitachukua beki mwengine.