Wenger aiomba Chile 'isimchezeshe' Sanchez

Alexis Sanchez Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexis Sanchez amefungia Arsenal mabao sita Ligi ya Premia msimu huu

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameiomba Chile kutomuweka hatarini mshambuliaji Alexis Sanchez mechi ya taifa hilo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay.

Sanchez, 27 ,alikosa mechi ambayo Chile walitoka sare 0-0 naColombia Alhamsii baada yake kupata jeraha la misuli.

Matabibu wa Chile wamekuwa wakitumai atapata nafuu kwa wakati kuweza kucheza mechi hiyo dhidi ya Uruguay Jumanne mjini Santiago.

"Huwa anapenda kucheza na kila wakati huwa tayari kucheza hata anapoumia," Wenger aliambia beIn Sports.

Sanchez, amefunga mabao manane mashindano yote msimu huu akichezea Arsenal.

Hakucheza miezi miwili msimu uliopita baada ya kuumia misuli ya paja.

"Ni kizungumkuti na lazima tulinde afya ya Alexis Sanchez," Wenger amesema.

"Lazima matabibu wetu waweze kuangalia uchunguzi wa MRI na kuona uzito wa jeraha na kuwa na uhakika kabisa kwamba uamuzi kuhusu kuchezeshwa kwake hautamwathiri siku za usoni."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Kuhusu BBC

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea