Mkufunzi wa Uingereza ataka kujua hatma yake

Kaimu mkufunzi wa Uingereza gareth Southgate
Image caption Kaimu mkufunzi wa Uingereza gareth Southgate

Kaimu mkufunzi wa Uingereza Gareth Southgate anataka kujua hatma yake katika kipindi cha mwezi mmoja iwapo shirikisho la soka nchini Uingereza FA litamuajiri kama kocha.

Mechi ya mwisho ya meneja huyo itakuwa ile ya kirafiki itakayochezwa siku ya Jumanne dhidi ya Uhispania katika uwanja wa Wembley.

Kamati ya FA itaamua ni nani atakayepewa kazi hiyo,huku Southgate akipigiwa upatu kuchukua wadhfa huo.

''Itakuwa muhimu kwangu mimi kujua ni nini nitakachofanya baada ya katikati ya mwezi Novemba '',alisema.