Kati ya Manchester United na Arsenal nani ataibuka mshindi?

Marcus Rashford alipofunga mabao mawili mwezi Februari Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marcus Rashford alipofunga mabao mawili mwezi Februari

Ligi ya premia inatarajiwa kuanza baada ya mapumziko ya kimataifa huku mechi kubwa ikiwa ni kati ya Manchester United na Arsenal Jumamosi uwanjani Old Trafford.

Southamton na Liverpool nao watakabiliana saa kumi na mbili jioni.

HABARI ZA TIMU

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic hatashiriki mechi moja baada ya kupigwa marufuku ya kutoshiriki mechi moja.

Wachezaji wanne wa United Luke Shaw, Marouane Fellaini, Antonio Valencia na Wayne Rooney wanauguza majeraha.

Arsenal inasubiri kufanya uamuzi kumhusu Alexis Sanchez, ambaye alishiriki mechi ya kwanza akiwa na Chile siku ya Jumanne licha ya jeraha la paja, mwanzoni mwa mapumziko ya kimataifa.

Beki wa kulia Hector Bellerin atakosekana kwa wiki nne kutokana na jeraha la kifundo cha mguu huku Santi Cazorla bado akisalia nje ya mchezo.

Wanachosema Meneja

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, kuhusu rekodi yake dhidi ya timu zilizoongozwa na Jose Mourinho: Mnafahamu huwa hatushindwi nyakati zote. Kuna baadhi ya mechi tumewashinda na nyingine tukatoka sare.

Kwa maoni yangu nimewashinda dhidi ya kila meneja ulimwenguni katika miaka 20 niliyokuwa hapa, na mchezo huu sitauchukulia kama wa ushindani kati ya meneja wawili.

Ni kati ya klabu mbili na timu mbili na naweza kuelewa kuwa watu wanataka kuzua vurumai, lakini si jambo linalomfanya mtu kuwa shabiki. Kile kitakacho mvutia shabiki ni kiwango cha mchezo.

Ukweli kuhusu timu

Arsenal hawajashinda katika mechi zao tisa ligi ya Premia katika uwanja wa Trafford, wamepoteza mechi saba katika mechi hizo.

Lakini, Gunners walishinda ugenini kwa United katika ya Kombe la FA mwaka 2015.

Manchester United

United wanaweza kutoka sare katika mechi yao ya tatu mfululizo katika ligi ya nyumbani kwa mara ya kwanza tangu mwezi wa Februari na April mwaka 1992.

Kushindwa kutawaacha na alama 18 baada ya mechi 12, na kufikia kiwango cha chini zaidi cha alama walichoweka Ligi ya Premia msimu wa 2004-05

Jose Mourinho hajawahi kupoteza kwenye ligi ya Premia dhidi ya Arsenal, amepata ushindi mara tano, na kutoka sare katika mechi 6 kati ya11 walipokutana na Gunners.

Wayne Rooney amefunga mara 14 katika mashindano yote dhidi ya Arsenal katika taaluma yake. Amekuwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao 15 dhidi ya Aston Villa.

Rooney alifunga goli lake la kwanza katika ligi ya Premia dhidi ya Arsenal, goli lake la 100 katika ligi ya Premia pia alilifunga dhidi ya Arsenal. Anahitaji mabao mawili kumfikia Bobby Charlton anayeongoza kwa ufungaji mabao akiwa na mabao 249 katika mashindano yote.

Arsenal

Arsene Wenger alishinda mechi yake ya kwanza kabisa kati ya mechi 15 alizochezesha timu dhidi ya Jose Mourinho mwaka 2015 katika shindano la michuano ya Community Shield.

Arsenal walichapwa mechi moja waliyocheza ugenini mwaka 2016, iliyochezwa katika uwanja wa Manchester United mwezi Februari.

Wamepoteza mechi moja kati ya mechi 21 walizoshiriki karibuni katika ligi kuu.

Gunners ni moja kati ya timu mbili katika ligi ya Premia ambazo hazijafungwa katika dakika 15 za kwanza za mchezo msimu huu, pamoja na West Brom.