Ndayisenga aelekea kushinda mbio za baiskeli "Tour of Rwanda

Image caption Valens Ndayisenga ashinda awamu ya  6 ya mashindano ya  mbio za baiskeli "Tour of Rwanda

Mnyarwanda  Valens Ndayisenga ameshinda awamu ya  6 ya mashindano ya  mbio za baiskeli "Tour of Rwanda  na kujihakikishia kunyakua taji la mashindano hayo.Ndayisenga ameshinda  awamu hiyo ya kilomita 109 kutoka Musanze hadi mjini Kigali kwa kutumia saa 3 dakika 20 na sekunde 38 akimshinda kwa tairi tu la baiskeli mwenzake wa timu ya Dimension Data ya Afrika kusini Eyob Metkel  kutoka Eritrea.Kesho ni mzunguko wa mwisho wa mashindano hayo mjini Kigali umbali wa kilomita 108.

Image caption Kesho ni mzunguko wa mwisho wa mashindano hayo mjini Kigali umbali wa kilomita 108.

Kwa matokeo ya ujumla Valens Ndayisenga ameweka tofauti ya sekunde 42 kati yake na Eyob Metkel anayeshikilia nafasi ya pili. Sekunde hizo zinatosha kumwezesha Valens Ndayisenga kunyakuwa  ushindi wa Tour of Rwanda kwa mara ya pili  baada ya kunyakua ushindi huo kwa mara ya kwanza mwaka 2014.