Mashabiki wa Man United wajificha chooni Old Trafford

Mashabiki wa machester United walijifica chooni katika juhudi za kutaka kutazama mechi kati Man United na Arsenal wikendi iliopita
Image caption Mashabiki wa machester United walijifica chooni katika juhudi za kutaka kutazama mechi kati Man United na Arsenal wikendi iliopita

Mashabiki wawili wa klabu ya Manchester United waliutumia usiku wa kuamkia mechi kati ya klabu hiyo na Arsenal katika choo cha uwanja wa timu yao katika juhudi za kutazama mechi kati ya klabu hizo mbili.

Mashabiki hao walikuwa wametembelea uwanja huo lakini baadaye wakajificha ndani ya choo hicho.

Walipatikana siku ya Jumamosi alfajiri wakati wa ukaguzi wa kiusalama kabla ya kukabidhiwa maafisa wa polisi ambao waliamua kutowakamata.

United imesema kuwa hakukuwa na tishio lolote la mashabiki walioingia katika uwanja huo kushabikia mechi hiyo.

Wawili hao walifanyiwa ukaguzi wa kisalama kabla ya kuingia katika uwanja huo kabla ya kuanza ziara yao uwanja huo.

Kisa hicho kinajiri miezi sita baada ya mechi ya ligi ya premia kati ya Manchester United na Bournemouth kusimamishwa kwa muda katika uwanja wa Old Trafford baada ya mfuko uliotuhumiwa kupatikana katika choo kilichoko katika kona ya uwanja huo.

Hatahivyo ilibainika kwamba kilikuwa kilipuzi bandia kilichowachwa baada ya zoezi mapema wiki hiyo.