Dennis Rodman ashtakiwa kwa kusababisha ajali

Deniss Rodman kushoto na Michael Jordan wakati awlipokuwa wakiichezea Chicago Bulls Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Deniss Rodman kushoto na Michael Jordan wakati awlipokuwa wakiichezea Chicago Bulls

Aliyekuwa nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani Dennis Rodman ameshtakiwa kwa kosa la kugonga na kutoroka ambalo lina hukumu ya kifungo kisichozidi miaka miwili.

Nyota huyo aliye na umri wa miaka 55 anatuhumiwa kwa kuendesha gari kwa kutumia barabara isiofaa huko kusini mwa jimbo la California ,swala lililolazimu gari jingine kukwepa na kugonga ukuta.

Waendesha mashtaka wanadaiwa kwamba Rodman baadaye alitoroka eneo hilo mnamo tarehe 20 mwezi Julai na kuwapa maafisa wa polisi habari za uongo.

Image caption Kim Jong Un na rafikiye Denis Rodman

Pia ameshtakiwa kwa kuendesha gari bila leseni. Wakili wa Rodman,Paul Meyer anasema kuwa ajali hiyo ilitokea katika eneo ambalo halina ishara za trafiki zinazoonekana.

Ameongezea kuwa Rodman alizuia ajali hiyo kwa kutogonganisha,kusimama na kuzungumza na watu waliokuwa ndani ya gari hilo.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea mnamo tarehe 20 mwezi Januari.

Rodman alishinda mataji mawili na klabu ya Detroit Pistons pamoja na ubingwa na timu maarufu ya Chicago Bulls katika miaka ya 90 akishirikiana na Michael Jordan.