Ranieri atumai Leicester watafana UEFA

Claudio Ranieri Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meneja wa Leicester City,Claudio Ranieri

Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri anamatumai klabu hiyo itapata "mafanikio ya ajabu,'' watakapo kutanana na Brugge katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya siku ya Jumanne

Ranieri amesema sare itawasaidia kufuzu kwa hatua ya 16 bora.

Mabigwa hao watetezi wa ligi Premia wamo kileleni katika kundi G baada ya kupata ushindi mara tatu na kutoka sare mara moja.

"Tuko na nafasi ya kuendelea katika michuano hii,'' amesema meneja huyo wa Leicester.

''Naiheshimu klabu ya Brugge sana na siamini hawana hata alama moja. Hucheza vizuri na kujitengenezea nafasi nzuri - ni jambo la kushangaza.''

Timu ya Leicester imefurahisha katika mechi yao ya kwanza katika mashindano ya soka ya mabingwa ya ligi ya Ulaya licha ya kutofana katika kulitetea taji lao la ligi ya Premia.

Wamo katika nafasi ya 12 baada ya kushindwa mara nne kati ya mechi saba za mwisho ikiwemo ile ya siku ya Jumamosi waliposhindwa na Watford.

''Lengo letu ni kujaribu kushinda mechi ya leo (Jumanne) na kurudi kushiriki katika ligi ya Premia na kujaribu kuimarisha nafasi yatu katika jedwali,'' Mwitaliano huyo aliongeza.

Mshambualiaji Islam Slimani, alyenunuliwa pesa nyingi na Leicester, hatashiriki mechi hiyo ambayo itachezwa katika uwanja wa King Power kutokana na jeraha la paja.

Beki wa kati Nampalys Mendy ana jeraha la kifundo cha mguu na mlinda lango Kasper Schmeichel anauguza jereha la mkono.

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Marc Albrighton akifungia Leicester

Brugge wako katika nafasi ya mwisho kundini katika ligi ya Bara ulaya msimu huu, kwa kupoteza mechi nne, na kufungwa mabao 10. Wamefunga bao moja pekee.

Watashiriki mechi dhidi ya Leicester wanaojaribu kuondoka bila kushindwa kwa mara tano mfululizo katika ligi ya barani ulaya.

''Ni huzuni kutoka bila alama yoyote, ni jambo ambalo watu wanatucheka ni jambo ambalo tunataka kuliangamiza kwa mara moja,'' amesema mshambuliaji Jelle Vossen Brugge aliyechezea Middlesbrough na Burnley hapo awali.

''Tuko karibu kufikia kiwango cha timu nyengine na tuna uhakika tutapata ushindi.''

''Leicester bado ni mabigwa wa ligi Uingereza, wanacheza mpira wa moja kwa moja na wana mbio na nguvu. Lazima tuwe na ari ya kucheza Soka. Hawakuiba taji hilo msimu uliopita, hawajapoteza kiwango katika mchezo wao.''

Brugge watamkosa Bjorn Engels, ambaye alipata jeraha la bega walipochapwa na Leicester miezi miwili iliyopita na Abdoulaye Diaby pia anauguza jeraha huku Ruud Vormer akiwa amepigwa marufuku.

Mada zinazohusiana