UEFA: Leicester City wang'ara mbele ya Club Brugge

Leicester iliutawala vyema mchezo huo
Image caption Leicester iliutawala vyema mchezo huo

Leicester city wamepata ushindi maridhawa wakati wa muendelezo wa ligi ya mabigwa barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya club Brugge.

Leicester wanahitaji alama moja tu kutinga hatua ya mtoano.

Image caption Leicester hawajapoteza mchezo wowote ligi ya mabingwa Ulaya

Mchezaji Shinji Okazaki alimaliza vyema kazi ya Christian Fuchs na kuandika goli la kwanza kwa kikosi hicho kinachonolewa na Muitaliano Claudio Ranieri.

Riyad Mahrez akaongeza goli la pili kwa penati murua ikiwa ni goli lake la nne ndani ya ligi ya mabigwa baada ya Marc Albrighton kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Leicester city hawashikiki katika ligi ya mabingwa Ulaya huku wakiwa wanaboronga EPL.

Image caption Dotmund wanakuwa timu ya nne kufunga magoli nane katika mchezo mmoja

Matokeo ya michezo mingine

Monaco 2-1 Tottenham

Borussia Dortmund 8-4 Legia Warsaw

Sporting 1- 2 Real Madrid

CSKA Moscow 1- 1 Bayer 04 Leverkusen

FC Copenhagen 0-0 FC Porto

Dinamo Zagreb 0-1 Olympique Lyonnais

Sevilla 1- 2 Juventus