Borussia Dortmund na Legia Warsaw wavunja rekodi

Borussia Dortmund Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dortmund ni klabu ya nne kufunga mabao manane mechi moja ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Klabu za Borussia Dortmund na Legia Warsaw zilivunja rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne, kwa kufungana jumla ya mabao 12.

Wajerumani hao chini ya Thomas Tuchel walishinda wapinzani wao kutoka Poland 8-4 mechi ya kusisimua iliyochezewa Ujerumani.

Walivunja rekodi iliyowekwa mabao 11 yalipofungwa mechi ambao Monaco waliwalaza Deportivo La Coruna 8-3 mwaka 2003.

Mabao saba yalifungwa dakika 22 za kipindi cha kwanza.

Legia ndiyo klabu ya kwanza kufunga mabao manne mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na bado kushindwa kwenye mechi.

Rekodi zilizovunjwa

  • Ni mara ya kwanza historia ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wachezaji wanane kufunga mechi moja
  • Dortmund ni klabu ya nne baada ya Liverpool, Monaco na Real Madrid kufunga mabao manane mechi moja Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
  • Ilikuwa mechi ya kwanza michuano ya ngazi ya juu Ulaya kufungwa magoli 12 tangu Ajax walipolaza Red Boys Differdange wa Luxemburg 14-0 michuano ya zamani ya Kombe la Uefa 3 Oktoba 1984.
  • Ni mechi moja pekee historia ya Kombe la Ulaya na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo mabao zaidi yalifungwa, Feyenoord ya Uholanzi ilipolaza KR ya Iceland 12-2 mnamo Septemba 1969.
  • Dortmund sasa wamefunga mabao 14 dhidi ya Legia msimu huu, mabao mengi zaidi kufungwa dhidi ya mpinzani mmoja msimu mmoja wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
  • Shinji Kagawa - ambaye wakati mmoja alichezea Manchester United - alifunga mabao mawili katika sekunde 76, mabao mawili ya kasi zaidi historia ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Reus arejea kwa kishindo

Marco Reus wa Dortmund alirejea kwa kishindo baada ya kukaa nje kwa miezi sita kutokana na jeraha. Alikuwa na nahodha wa timu na alifunga mabao matatu.

"Nilifurahia kuwa hapo tangu mwanzo," alisema Reus ambaye alikosa Kombe la Dunia 2014 na Euro 2016 kutokana na jeraha.

Mamo yalivyokuwa

Moja - Legia wajiweka kifua mbele

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aleksandar Prijovic afungia Legia Warsaw bao la kwanza dakka ya 10

Mbili - lakini hawaongozi muda mrefu

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shinji Kagawa asawazisha dakika ya 17, kisha milango inafunguka

Tatu - Wajerumani wanaongoza

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dakika moja baadaye, anafunga la pili na kuwaweka Dortmund kifua mbele

Nne - nakuongeza jingine

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dakika tatu baadaye, Nuri Sahin anamwadhibu kipa wa Legia baada yake kufanya kosaarted...

Tano - lakini Legia wanakomboa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Prijovic anafunga la pili (na kufanya mambo 3-2). Hilo ni bao la nne katika dakika saba

Sita - sasa ni 4-2, wataendelea?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ousmane Dembele afungia Borussia Dortmund la nne dakika ya 29

Saba - Reus anafanya mambo

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marco Reus, ambaye anacheza mara ya kwanza baada ya kukaa nje miezi sita kutokana na jeraha, anafunga lake la kwanza dakika ya 32

Nane - na kisha anafunga jingine

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption ... na lake la pili dakika ya 52. Mambo bado ....

Tisa - watajikwamua?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Michal Kucharczyk wa Legia ajaribu kuwamkwamua, anafunga dakika ya 57 na mambo yanakuwa 6-3. Lakini Dortmund wanaendeea kutamba

Kumi - tumefikisha mabao kumi!

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Baada ya kipindi cha utulivu, cha dakika 24 bila goli, Felix Passlack wa Dortmund anaibuka na uwafungia la saba.

11 - umekuwa usiku mrefu?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bao la Nemanja Nikolic linafanya 7-4, lakini mashabiki wa Legia wanaonekana kuzidiwa, wamevua tisheti zao karibu wote.

12- mambo yanamalizika 8-4

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nahodha wa Dortmund anakamilisha mambo kwa bao lake la tatu usiku huo - hat-trick! Usiku wa historia!

Mada zinazohusiana