Marekani: Arena kumrithi Klinsmann kama meneja

Bruce Arena Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bruce Arena

Bruce Arena, ameteuliwa kuwa meneja mkuu wa timu ya taifa ya Marekani kwa mara ya pili, kumrithi Jurgen Klinsmann aliyepigwa kalamu siku ya Jumatatu

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 65, anayeiaga timu ya LA Galaxy, kuchukua nafasi hiyo, aliongoza nchi yake mwaka 2002 hatua ya robo fainali alipoanza kuhudumu kwa mara ya kwanza.

Arena pia aliongeza kiwango cha ushindi kwa mameneja wa Marekani, kwa kupata ushindi mara 71 kati ya michezo 130 katika miaka ya 1998 na 2006.

Pia ameshinda vikombe vitano katika ligi ya MSL akiiongoza timu ya LA Galaxy ya jiji la New York na DC United.

Klinsmann,52, aliiongoza timu ya Marekani kuwa miongoni mwa timu 16 bora katika Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil, lakini wamepoteza michezo miwili ya kufuzu kwa michuano ya mwaka 2018.

Marekani wamo katika nafasi ya mwisho ya nchi sita zinazoshindania kufuzu Kombe la Dunia kutoka bara la Amerika, nyuma ya mataifa madogo kama vile Panama na Honduras.

"Ukipata nafasi ya kuwa meneja wa timu ya taifa ,ni heshima,'' Arena amesema.

Ninauhakika tutachukua hatua zifaazo na kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa Urusi mwaka 2018.

Arena atachukua hatamu ya kuwa meneja tarehe 1 mwezi Disemba,na mechi yake ya kwanza itakuwa nyumbani dhidi ya Honduras tarehe 24 mechi mwaka 2017.

Mada zinazohusiana