Arsenal nyuma ya PSG hatua ya makundi

Timu ya Arsenal watoka sare na PSG Haki miliki ya picha EPA
Image caption Arsenal wamefuzu kwa hatua ya muondoano mara ya 14 mfululizo

Arsenal wanakabiliwa na kibarua kumaliza wakiwa wanaongoza kwenye kundi lao mechi za Kombe la Klabu Bingwa Ulaya baada ya kutoka sare na Paris St-Germain (PSG) katika uwanja wa Emirates Jumatano usiku.

Gunners walitaka ushindi ili kuwawezesha kuwa kileleni katika kundi A baada ya miaka mingi kumaliza wa pili na kuondolewa mara sita katika timu 16 bora katika hatua ya muondoano.

Edinson Cavani alipata bao la kwanza katika dakika ya 18.

Olivier Giroud, alifunga penalti kabla ya mapumziko baada ya Grzegorz Krychowiak kusababisha ikabu kwa kumchezea visivyo mshambuliaji Alexis Sanchez. Marco Verratti alifunga bao la pili katika dakika 60.

PSG pia walikuwa hatari huku Lucas akipiga mpira wa kichwa uliomgusa Alex Iwobi na kuwawezesha kusawazisha katika dakika ya 77.

Cavani alikosa nafasi mbili nzuri za kufunga.

Ingawa Arsenal na PSG wana alama sawa kila mmoja akiwa amesalia na mechi moja, mabingwa hao wa Ufaransa wana nafasi bora kwa kuzingatia matokeo baina ya klabu hizo mbili.

PSG walifunga mabao mengi ugenini, Emirates kwenye sare hiyo ya Jumatano. Klabu hizo zilipokutana Paris, zilitoka sare ya 1-1, hivyo Arsenal wana bao moja pekee la ugenini mechi baina ya klabu hizo.

Kukosa kwa Arsenal kuongoza hatua ya makundi kumewasababishia kupangwa na klabu hatari, zinazoongoza makundi, na hivyo kushindwa kupita hatua ya 16 bora kwa miaka 7.

PSG watakutana na Ludogorets katika mechi yao ya mwisho, timu ambayo Arsenal iliichapa mabao 6-0 , huku Wenger na vijana wake wakielekea Basel.

Mada zinazohusiana