Steven Gerrard astaafu katika soka

Steven Gerrard astaafu soka
Image caption Steven Gerrard astaafu soka

Aliyekuwa nahodha wa Liverpool na timu ya Uingereza Steven Gerrard amestaafu na kukamilisha miaka 19 ya kucheza soka.

Gerrard mwenye umri wa miaka 36 aliichezea Liverpool mara 710 na kushinda mataji manane makuu ,lakini akajiunga na klabu ya LA Galaxy ya ligi ya MLS nchini Marekani mwaka 2015.

Kiungo huyo wa kati ni mchezaji wa nne kuichezea mara nyingi Uingereza baada ya kucheza mara 144 mbali na kuwa nahodha wa timu hiyo ya taifa katika mashindano matatu kati ya sita aliyoshiriki.

''Ni bahati kubwa kushiriki katika michuano mingi wakati nilipokuwa nikisakata kandanda'',alisema Gerrard

"Nimekuwa na muda mzuri na nashkuru kwa wakati wote wa muda wangu katika timu ya Liverpool ,Uingereza na LA Galaxy.Nilifanikisha ndoto yangu ya utotoni kwa kuichezea Liverpool''.