Ibrahimovic: Rooney anastahili heshima

Wachezaji wa Manchester United Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa Manchester United

Mshambuliaji wa Manchester united Zlatan Ibrahimovic, amesema Wayne Rooney''ni mchezaji bora'' na anastahili heshima zaidi, baada ya nahodha huyo wa Uingereza kuvunja rekodi ya ufungaji mabao.

Manchester United walifunga mabao 4-0 dhidi ya Feyenoord kwenye ligi ya Europa iliyochezwa siku ya Alhamisi.

Rooney, mwenye umri wa mika 31, alifunga goli la 39 barani Ulaya na kuifanya United kupata alama katika fainali ya hatua ya makundi dhidi ya Zorya Luhansk itakayowafikisha katika timu 32 bora katika ligi ya Europa.

Hii ni kutokana na mchango wa Rooney, ambaye amesalia na goli moja kufikia rekodi ya Sir Bobby Charlton ya magoli 249.

''Ni mtu mzuri , Ibrahimovic, aliyemsaidia Rooney kufunga bao la kwanza, aliambia BBC Sport. Nafurahi kwa kuwa amevunja rekodi. Lakini nitamsaidia kupata bao jingine. Lile ambalo litamfanya kuweka rekodi ya ukweli.''

Rooney aliomba radhi wiki iliyopita kwa picha ambazo ''hazifai'',alipohudhuria harusi katika hoteli walimokuwa ikilala timu ya taifa wakati wa mapumziko ya kimataifa.

Lakini Jumamosi alisema ripoti hizo ''zilikosa heshima'',akiongezea:Ni kama vyombo vya habari vinajaribu kuandika matangazo ya kifo change.

Alikasirika alipoulizwa tena swali kuhusiana na picha hizo baada ya ushindi dhidi ya Feyenoord, alisema: Kile kinachobuniwa na watu kama wewe unayeuliza maswali, kuyafanya mambo kuwa makubwa bila sababu yoyote.

''sikuhudhuria harusi hiyo,na ni aibu kuzungumzia kuhusu hilo usiku kama wa leo.''

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic

Ibrahimovich alisema:'' Kwa mafikira yangu mtu akiwa na umaarufu kama hivyo, watu hutaka kujua zaidi kukuhusu.''

Tunastahili kumshukuru kwa kuwa michezaji jinsi alivyo, kwa kile alichokifanya. Siwaoni wachezaji wengi kutoka Uingereza walio na taaluma kama yake. Wanastahili kumpa heshima. Kila mtu hupenda kufanya jambo dogo kuwa kubwa.

Meneja Jose Mourinho alisema: Watu kama yeye hawastahili kujibu chochote tena , anastahili kufurahikia miaka michache iliyosalia katika taaluma yake na kucheza mchezo mzuri kadri ya uwezo wake.