Simba vs Yanga: Simba yataka refa kutoka nje

Simba dhidi ya Yanga
Image caption Simba dhidi ya Yanga

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Simba kufuata kanuni na taratibu za shirikisho,

Kauli hiyo ya TFF inafuatia ile kauli ya Simba ya kusisitiza kuwa inataka waamuzi kutoka nje ya nchi na kama TFF isipofanya hivyo, watakapokutana na watani wao wa jadi Yanga, hawatapeleka timu uwanjani.

Kwa mujibu wa msemaji wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amesema wao wataendelea kuwatumia waamuzi wa Tanzania na kama Simba hawatapeleka timu, wao wanasubiri kuchukua hatua kali za kinidhamu.

Kupitia kikao chao na waandishi wa habari, msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema wao hawatapeleka timu hadi TFF itakapotumia waamuzi kutoka nje ya Tanzania kwenye mchezo wao dhidi ya watani wao wa jadi kwa kuwa waamuzi wa ligi kuu ya Tanzania wamekuwa hawachezeshi kwa haki hasa Simba inapokutana na Yanga.