Wasiwasi Arsenal kuhusu jeraha la Debuchy

Mathieu Debuchy Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Mathieu Debuchy alikaa kwa mkopo kwa muda Bordeaux msimu uliopita

Beki wa kulia wa Arsenal Mathieu Debuchy ana wasiwasi kwamba jeraha alilolipata Jumapili ni mbaya, meneja Arsene Wenger amesema.

Debuchy, 31, alichezea Gunners mara ya kwanza tangu Novemba 2015 mechi ya Ligi ya Premia dhidi ya Bournemouth ambayo walishinda 3-1 lakini akaumia misuli ya paja na kulazimika kuondoka uwanjani baada ya dakika 16 pekee.

Arsenal walisinda kupitia mabao mawili ya Alexis Sanchez na moja la Theo Walcott.

"Itanibidini kuzungumza na matabibu, lakini unaweza tu kujua hali halisi baada ya saa 48," alisema Wenger.

"Unahitajika kuacha damu itoke kisha baadaye tuwe na uchunguzi wa MRI baada ya saa 48 kubaini ubaya wa jeraha."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Kuhusu BBC

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea