Mourinho hatarini ya kuadhibiwa na FA

Jose Mourinho Haki miliki ya picha Reuters and Getty Images
Image caption Jose Mourinho alitumikia marufuku ya mechi moja dhidi ya Swansea chini ya mwezi mmoja uliopita

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anakabiliwa na uwezekano wa kuadhibiwa tena na Chama cha Soka Uingereza (FA) baada ya kufukuzwa uwanjani na refa Jumapili.

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwake kufukuzwa uwanjani na mwamuzi katika kipindi cha mwezi mmoja.

Mreno huyo alifukuzwa na mwamuzi Jon Moss baada yake kuonekana kukerwa na uamuzi wa refa huyo wa kumuonesha Paul Pogba kadi ya manjano kwa kujiangusha uwanjani mechi ya dhidi ya West Ham, na akapiga chupa teke kwa hasira.

Mechi hiyo ilimalizika sare 1-1.

Video zinaonesha mchezaji wa West Ham Mark Noble hakumgusa Pogba hata kidogo.

Mourinho, pia alifukuzwa uwanjani mwezi uliopita na refa Mark Clattenburg wakati wa mechi iliyomalizika sare 0-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Burnley.

Alitumikia marufuku ya mechi moja wakati wa mechi dhidi ya Swansea.

Katika kisa kingine, alitozwa faini ya £50,000 kwa tamko lake kuhusu mwamuzi Anthony Taylor kabla ya mechi kati ya Manchester United na Liverpool.

Moss pia alimfukuza uwanjani Mourinho Oktoba 2015 Mreno huyo alipokuwa anaikufunza Chelsea wakati wa mechi dhidi ya West Ham.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mourinho akipiga chupa teke wakati wa mechi dhidi ya West Ham
Matokeo ya Manchester United baada ya mechi 13 ligini... Meneja
2016-17: alama 20, nambari sita Jose Mourinho
2015-16: alama 27, nambari mbili Louis van Gaal
2014-15: alama 22, nambari nne Louis van Gaal
2013-14: alama 22, nambari nane David Moyes

Man Utd waendelea kudidimia

Mambo yanaendelea kuwa mabaya...
Manchester United sasa wameshindwa kupata ushindi mechi nne za ligi mfululizo Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu Februari 1990
Na pia wametoka sare nyumbani mechi nne mfululizo nyumbani kwa mara ya kwanza tangu Desemba1980.