Barry Bennell akutwa hoi ,alazwa hospitalini

Uingereza
Image caption Barry Bennell

Imefahamika kuwa kashfa ya kuwanyanyasa kingono watoto wadogo na kuzidi kulitia doa soka la Uingereza ambalo wiki za hivi karibuni mwanasoka huyo imefahamika kwamba yuko hospitalini, baada ya taarifa za kutoonekana kwake.

Polisi wa uingereza wamekaririwa wakisema kwamba wamemkuta Barry Bennell akiwa hajitambui hospitali katika anuani ya kaskazini mwa London, baada ya taarifa hiyo polisi hawakuendelea kueleza ikiwa Barry alikuwa amefanya jaribio la kukata kukatisha uhai wake.

Barry Bennell awali aliwahi kufungwa gerezani mara tatu nchini Uingereza na Marekani kwa makosa ya ya kingono kwa watoto mnamo miaka ya 1970.

Tayari polisi nchini Uingereza imeanza kufanya uchunguzi madai ya wachezaji kadhaa wa zamani vijana kwamba waliwahi kunyanyaswa kingono pindi walipokuwa wavulana wadogo .

Nao Umoja wa Vyama vya Soka barani Ulaya umetoa tamko kuwa aina yoyote ya tabia za unyanyasaji katika soka hazikubaliki kabisa.