Coutinho:Kusalia nje hadi Januari

Philippe Coutinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho amefunga magoli sita kwa Liverpool msimu huu

Mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho alifanyiwa uchunguzi wa kifundo cha mguu siku ya Jumatatu huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda atakuwa nje ya mchezo hadi katikati mwa mwezi Januari mwaka ujao.

Coutinho, 24, alitolewa uwanjani kwenye machela baada ya kugongana na mchezaji wa Sunderland Didier Ndong, katika kipindi cha kwanza cha mchezo siku ya Jumamosi walipotoka na ushindi wa magoli 2-0 katika uwanja wa Anfield.

Ingawaje matokeo kamili kuhusu uchunguzi huo hayajabainika, kuna uwezekano raia huyo wa Brazil aliumia kwenye kano za mguu.

Jeraha kama hilo huwafanya wachezaji kukaa nje kwa wiki tano au sita.

Ni bayana kwamba mchezaji huyo maarufu wa Jurgen Klopp,Coutinho atarudi katika sehemu ya pili ya ligi ya Premia, na kwamba atakosa michezo muhimu.

Liverpool watakutana na Everton katika debi ya Merseyside,uwanjani Goodison Park tarehe 19 Disemba, na tarehe 31 watakutana na Manchester City katika uwanja wa Anfield.

Haki miliki ya picha Getty Images

Coutinho anauwezekano wa kukosa kushiriki michezo hiyo miwili iwapo atathibitishwa kuwa na jeraha hilo.

Alikuwa katika uwanja wao wa mafunzo wa Liverpool Melwood siku ya Jumapili,ambapo alionekana akiondoka katika uwanja huo kwa magongo huku fundo lake la mguu wa kulia likiwa umevalishwa viatu maalum kabla ya kufanyiwa uchunguzi saa 24 baadaye.

Klopp pia atamkosa Sadio Mane, aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 34 mwezi Januari.

Mane atakuwa akihudhuria mechi ya kuwania Kombe la Mataifa Bingwa Afrika nchini akichezea taifa lake Senegal.

Mjerumani huyo pia inatarajia kumkosa Roberto Firmino siku ya Jumanne katika robo fainali ya ligi ya EFL dhidi ya Leeds United katika uwanja wa Anfied baada yakupata jeraha la misuli dhidi ya Sunderland.

Daniel Sturridge ambaye alikosa mechi hiyo ya Jumamosi baada ya kupata shida ya misuli ya chini mguuni naye pia hataweza kucheza Jumanne.

Adam Lallana ambaye amekosa mechi mbili za Liverpool za ligi ya Premia kutokana na jeraha walipokuwa wakimenyana na Uhispania na kutoka sare ya mabao 2-2 huko Wembley, anaendelea kupata nafuu.

Lallana, anaendelea na mazoezichini ya kocha wa mazoezi wa Liverpool, lakini hatashirikishwa miongoni mwa wachezaji watakaoshiriki mechi hiyo dhidi ya Leeds.