Timu ya bunge la Tanzania kambini

Tanzania Haki miliki ya picha Google
Image caption Mwenyekiti wa timu ya Bunge,William Ngereja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza.

Kikosi cha timu ya Bunge la Tanzania kilichosheheni wachezaji wa michezo ya mpira wa miguu,wavu,riadhaa ,kuvuta kamba na mchezo wa gofu ambacho kinajumuisha wachezaji 60 ambao watashiriki kwenye mashindano yanayotazamiwa kuwa na ushindani mkubwa .

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga mara baada ya timu hiyo kutua,Mwenyekiti wa timu ya Bunge,William Ngereja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza alisema kuwa maandalizi kwa upande wa timu yao yamekamilika kwa asilimia kubwa.

Alisema kutokana na umuhimu wa mashindano hayo waliamua kuweka kambi mkoani Tanga ili kuendana na hali ya hewa kabla ya kwenda nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ikiwa ni mpango wa kuimarisha kikosi chao.

"Mimi nisema tu sisi kama timu ya Bunge nia na lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye mashindano hayo na ndio maana tumeamua kuweka kambi mkoani Tanga lakini pia hata hivyo pia kikosi chetu kimeimarika kutokana na usajili ambao tumekuwa tukiufanya kila baada ya miaka mitano "Alisema Ngeleja.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la timu ya Bunge,Stephen Ngony'ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu alisema kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Alisema timu hiyo ipo kwenye mazingira mazuri ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mashindano hayo ili kuweza kutimiza dhamira yao waliojiwekea ya kutwaa ubingwa.

Kwa upande wake,Nahodha wa timu ya Mpira wa Pete ya Bunge,Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kawe kwa tiketi ya chama cha CHADEMA, alisema kuwa wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanafanya vizuri ili kutimiza dhamira waliojiwekea ya kuibuka na Ubingwa."Sisi kama timu ya mpira wa Pete ya Bunge tumejipanga vizuri na kikosi chetu kina ari kubwa ya kuhakikisha tunaiwakilisha nchi yetu ya Tanzania ipasavyo kwa mafanikio makubwa"Alisema. habari na Tanga Raha