Arsenal kuwakosa Giroud na Debuchy

Mshambuliaji wa Arsenal Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Oliver Giroud

Mshambuliaji wa Arsenal Mfaransa Oliver Giroud ataukosa mchezo wa ligi dhidi ya Southampton na kuwa majeruhi.

Nyota mwingine atakakosa mchezo huo ni beki Mathieu Debuchy anayesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa Debuch lifanyiwa vipimo lakini bado majibu hayatoka.

Mshambuliaji Lucas Perez anatarajiwa kuanza baada ya kupona maumivu ya enka yaliyomuweka nje kwa wiki tano.