Diafra Sakho nje ya uwanja miezi sita

Ulaya Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mshambuliaji wa West Ham United Diafra Sakho

Mshambuliaji wa West Ham United Diafra Sakho atakua nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita kwa sababu ya maumivu ya paja.Sakho mwenye umri wa miaka 26, alitolewa uwanja dakika ya 66, katika mchezo wa ligi kuu ya Englandi timu yake ilipocheza na Man United.

Mchezaji huyu alirejea uwanjani katika mchezo huo baada ya kuwa majeruhi kwa muda na kuifungia timu yake bao la kuongoza.

Kocha wa West Ham Slaven Bilic amesema "Ni pigo kubwa kwetu," Kuumia kwa nyota huyu wa timu ya taifa ya Senegal kunatia mashaka kama ataweza kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya africa itayofanyika mwezi January 2017.