Fainali: Kina dada wa Cameroon kukutana na Nigeria

Kikosi cha Cameroon

Fainali ya awamu ya kumi ya Kombe la Mataifa ya Afrika miongoni mwa kina dada, imerudia matokea yake ya awamu ya tisa iliyochezwa nchini Namibia, ambapo Nigeria iliichapa Cameroon mabao 2-0.

Mechi ya fainali inatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Ahamadou Ahidjo, mjini Yaounde huku rais Paul Biya akitarajiwa kuwa miongoni mwa mashabiki wengi watakaohudhuria mechi hiyo.

Kina dada kutoka Nigeria Super Falcons wanatarajia kulitetea taji lao kwa kupata ushindi wa mara ya nane kati ya mechi 10 walizoshiriki.

Timu ya Cameroon ya Indomitable Lionesses wanatafuta kupata ushindi kwa mara ya kwanza katika kombe la Taifa, mechi ambayo itakuwa mechi yao ya fainali ya tatu.

Timu hizo mbili zilipitia ushindani mkali katika nusu fainali walipotoka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.

Cameroon inatarajiwa kupata goli moja katika shindano hilo, huku Nigeria wamefunga magoli 12.

Haki miliki ya picha Getty Images

Super Falcons wameziba nyavu yao na kukubali bao moja ambalo lilifungwa kupitia mkwaju wa penalti dhidi ya Ghana .

Cameroon wamefunga mabao sita, lakini ilitarajiwa kupata mabao zaidi kutokana na umiliki wa mchezo waliouonyesha uwanjani.

Nahodha msimamizi wa Cameroon, Augustine Ejangue, amesema wachezaji chipukizi wa timu hiyo wako tayari kumenyana kwenye fainali na kuna mshikamano halisi kwa kikosi chote hicho cha Cameroon.

Kocha wa Nigeria, Florence Omagbemi, anatarajiwa kuwa kocha mwanamke wa pili kushinda taji hilo. Omagbemi alishinda taji la kwanza kama nahodha. Amesema kikosi chake kiko tayari kiakili, kimwili na kisaikolojia kuhifadhi taji lao.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Asisat Oshoala

Nyota wawili katika mashindano hayo ya soka ya kina dada nchini Afrika watakutana ana kwa ana kwenye fainali na mchezaji wa Nigeria na Arsenal Asisat Oshoala, ataongoza kikosi cha mashambulizi cha Super Falcons naye Rosengard's Gaelle Enganamouit wa Cameroon akiwa kiungo muhimu kwa Indomitable Lionesses.

Umati mkubwa wa mashabiki wataungana wakiwashabikia wenyeji Cameroon siku ya Jumamosi mchana.