Chelsea yairambisha sakafu Manchester City ugenini

Eden Hazard asherehekea bao lake la tatu wakati Chelsea ilipoinyuka Manchester City 3-1 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard asherehekea bao lake la tatu wakati Chelsea ilipoinyuka Manchester City 3-1

Ushindi wa Chelsea wa nane mfululizo katika ligi ya Uingereza uliimarisha azma yao ya kusalia katika uongozi wa ligi hiyo ,licha ya ushindi wao katika uwanja wa Etihad kukamilika kwa ghasia huku mshambuliaji wa City Sergio Aguero na Fernandinho wakitolewa nje katika muda wa majeruhi.

Kikosi cha Antony Conte kilitoa onyo kali baada ya kuicharaza City 3-1 licha ya kuwa nyuma kupitia bao la beki wake Gary Gahil aliyejifunga katika kipindi cha kwanza cha mechi.

Kevin de Bryune alipiga mwamba wa goli kunako dakika ya 56 kufuatia krosi maridhawa iliopigwa na Jesu Navas huku City wakidhibiti mchezo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola akishangazwa na mechi hiyo ilivyopinduka

Lakini Chelsea walipata bao la kusawazisha wakati Diego Costa alipomshinda nguvu Nicolas Otamendi na kufunga ,na kuongeza bao la pili dakika kumi baadaye baada ya mchezaji wa ziada Wilian kukimbia na mpira kabla ya kufunga kwa urahisi.

Nyota wa Chelsea Eden Hazard alikamilisha ushindi muhimu wa Chelsea baada ya kufunga bao jingine baada ya kumpita beki Aleksander Kolarov na kucheka na wavu.

Wachezaji wa City hatahivyo walikasirishwa na kile walichodai ni upendeleo wa refa Anthony Taylor baada ya Aguero kumchezea visivyo Luiz baada ya beki huyo kukabilana na mshambuliaji huyo wa kutegemewa hapo awali.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa Chelsea wakikabiliana na wenzano wa Manchester City katika mechi hiyo ya siku ya Jumamosi

Mchezaji wa Chelsea Nathaniel Chalobah aliingilia vita hivyo na alibahatika alipokosa kupewa kadi nyekundu ,huku Fernandinho akipewa kadi nyekundu kwa kumshambulia Cesc Fabregas.