Sanchez afunga Hat-trick, Arsenal yailaza West Ham

Alex Sanchez akimfunga kipa Darren Randolph wa West Ham Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alex Sanchez akimfunga kipa Darren Randolph wa West Ham

Alexi Sanchez alifunga hat-trick na kuisaidia timu yake ya Arsenal kuinyamazisha West Ham huku timu hiyo ikipanda hadi nafasi ya ya pili katika ligi ya Uingereza.

Mesut Ozil aliiweka kifua mbele Arsenal baada ya Angelo Ogbonna kufanya masikhara na kumpa fursa Sanchez kutoa pasi safi kwa Ozil.

West Ham ilitishia kusawazisha baada ya mapumziko ya kipindi cha kwanza kabla ya Sanchez kuingia katika eneo la hatari kuchenga na kucheka na wavu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexi sanchez aligunga mabao matatu na kuorodheshwa mchezaji bora katika mchi hiyo

Raia huyo wa Chile aliongeza bao la pili dakika nane baadaye kupitia kombora la kimo cha kuku ambalo lilimwacha kipa Darren Randolph bila jibu,kabla ya mshambuliaji wa West Ham Andy Caroll kuingia na kufunga mpira wa adhabu uliopigwa na Dimitri Payet na kugonga chuma cha goli la Arsenal.

Hatahivyo ,matumaini ya West Ham yalididimizwa na Alex Oxlaide Chamberlain aliyefunga bao la nne na Sanchez kufunga la tano .

Matokeo mengine ya ligi ya Uingereza

Crystal Palace 3 Southampton 0

Stoke 2 Burnley 0

Sunderland 2 Leicester 1

Tottenham 5 Swansea 0

West Brom 3 Watford 1