El Classico: Real Madrid yaizuia Barcelona

Sergio ramos wa Real Madrid akiisawazishia timu yake Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sergio ramos wa Real Madrid akiisawazishia timu yake kupitia kichwa

Nahodha wa Real Madrid alifunga kunako dakika ya mwisho ya mechi ili kuisawazishia timu yake na kuendeleza msururu wa kutofungwa msimu huu mbali na kuipokonya ushindi Barcelona katika mechi ya El Classico iliojaa hasira.

Kichwa cha Luiz Suarez kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Neymar kiliiweka Barcelana kifua mbele katika uwanja wa nyumbani wa Nou Camp.

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Jedwali la ligi ya Uhispania

Lakini mechi ikielekea kukamilika Cristiano Ronaldo alikosa bao la wazi kabla ya Ramos kusawazisha kupitia kichwa baada ya Luka Modric kupiga mkwaju wa adhabu na kuipatia alama moja timu hiyo ya Zinedine Zidane inayoongoza jedwali la ligi.

Viongozi hao sasa wako pointi sita juu ya mabingwa watetezi wa ligi Barcelona baada ya kucheza mechi 14.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sanchez akiifungia bao la kwanza timu yake katika mechi ya El Classico dhidi ya Real Madrid